Watu
wawili wamefariki dunia mkoani Simiyu katika matukio tofauti akiwamo
mtoto wa miezi mitatu aliyenyakuliwa na fisi akiwa mgongoni mwa mama
yake.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu, Gemin Mushy jana alisema kuwa
mtoto Ng’wanza Samwel, akiwa amebebwa na mama yake alinyakuliwa na
fisi Mei 25, majira ya saa 1;30 jioni katika kijiji cha Ngugunu,Tarafa
ya Kisesa wilayani Meatu.
Alisema katika kufuatilia tukio hilo, mabaki ya mtoto huyo yalipatikana
mita 200 tu fisi kutoka eneo alilonyakuliwa huku kichwa, kifua, tumbo,
mikono na miguu ikiwa haipo.
Katika tukio jingine mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la Magina
Supa(20), mkazi wa Nyaumata mtaa wa Kisiwani wilayani Bariadi, aliuawa
kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na bega la kushoto na mtu
aliyekuwa amempakiza kama abiria wake.
Akifafanua, Kamanda Mushy alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 26
majira saa 1;00 jioni katika mtaa wa Izunya, kata ya Somanda tarafa ya
Ntuzu wilayani Bariadi kwa mtuhumiwa wa mauaji hayo anayedaiwa kuwa
abiria wa mpanda baiskeli huyo aliyekuwa anajishughulisha na biashara
ya daladala ya baiskeli.
Kamanda huyo alisema kuwa mara baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa ambaye
hajafahamika na anasakwa baada uhalifu huo alitoroka. Chanzo cha mauaji
hayo hakijafahamika.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI