Hifadhi moja ya wanyama huko Japan
imelazimika kuomba radhi baada ya wahudumu wake kumpa tumbili mtoto wa kike, jina sawa na lile la mwanawe mwanamfalme wa Uingereza Charlotte.
Kituo
hicho cha wanyama cha Takasakiyama kilicho kusini mwa taifa hilo
kilikabiliwa na gadhabu kuu ya watu baada ya kumpa tumbili huyo wa kike
jina hilo sawa na binti mfalme wa Uingereza.
Chombo cha habari cha Kyodo kiliripoti tukio hilo kikidai kuwa raia waliihusika katika kuchagua jina la tumbili huyo wa kike.
''ni kawaida kwa tumbili wa kwanza kila mwaka kupewa jina na umma'' Kyodo
Jina hilo la Charlotte ndilo lililotokea kupendwa na watu wengi huku watu 59 kati ya raia 853 wakiipigia kura.
Baadhi ya raia walipinga pendekezo hilo wakisema haifai kuipa tumbili huyo jina sawa na binti mfalme.
Wengine walisema kuwa haitakuwa vyema kwao wenyewe iwapo waingereza wataita tumbili wao majina sawa na ya wafalme wao.
Kituo
hicho cha Wanyama kilichapisha taarifa kwenye mtandao wao wakiomba
msamaha huku wakipanga mikakati ya kubadilisha jina la tumbili huyo.