WATU SITA WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUPIGWA BOMU HUKO MOROGORO

Hofu ya ugaidi  imezidi kutanda katika wilaya ya Kilombero  baada ya watu  sita  kujeruhiwa vibaya na bomu lililorushwa kwa mkono  wakati wakitoka katika  maadhimisho ya Mei Mosi  katika kijiji cha Msolwa ujamaa kata ya Sanje  wilayani Kilombero mkoani Morogoro .


Katika hospitali ya ST Kizito Mikumi  walikolazwa majeruhi wa tukio hilo  wamesema  bomu hilo lilirushwa na vijana wawili   baada ya kutiliwa shaka na wananchi wa kijiji cha Msolwa Ujamaa kata ya Sanje tarafa ya Mangula kuwaweka chini ya ulinzi kwa ajili ya kuwapekua.

Kufuatia hali hiyo vijana hao walirusha  bomu  na kujeruhi wananchi pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwa kwenye gari la mwenyekiti wa halmashauri wakitokea katika maadhimisho ya Mei Mosi.

Wananchi hao wameomba jeshi  la polsi kufanya uchunguzi kufuatia matukio  yanayoashiria ugaidi kuendelea kuandama wakazi  wa Kilombero.


 Nao viongozi wa kata akiwemo diwani wa kata ya Sanje David Ligazio wamesema ipo haja ya serikali kuongeza nguvu ya jeshi la polisi ikiwa ni pamoja na magari ya usafiri na kutafuta vifaa vinavyo weza kuchunguza maeneo ya milima ya Udzungwa na Ruaha   ambapo wamebaini  wahalifu wengi  wamewaona wakitokea katika misitu hiyo  mara kwa mara.


Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard Paul  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema hadi sasa jeshi la polisi linawatafuta watuhumiwa  hao ambao baada ya kurusha bomu hilo limejeruhi dereva wa  mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero  na kuharibu gari ya halmshauri pamoja na wananchi wa kijiji cha Msolwa Ujamaa.


Tukio hilo limetokea ndani ya siku 14 baada ya watuhumiwa  9 kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi, bendera nyeusi pamoja na vitu mbalimbali vya kufanyia uhalifu huku mmoja akichomwa moto na wananchi wenye hasira akiwa katika harakati za kutoroka baada ya kumchoma askari kwa jambia shingoni katika   tarafa yaKidadu wilayani Kilombero.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post