Makundi hasimu ya askari
yanakabiliana katikati mwa mji mkuu wa Burundi- Bunjumbura, mahala
ambapo tangazo lilitolewa jana Jumatano kuwa Rais Pierre Nkurunziza,
amepinduliwa.
Radio na runinga ya taifa inang'ang'aniwa kwa sasa huku wanajeshi waaminifu kwa rais Nkurunziza ndio wanaoidhibiti.
Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza.
Rais huyo
ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa
kanda,baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.
Ingawa
askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi
yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya
rais wao,na kwamba udhibiti wan chi uko mikononi mwao na hasa katika
maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo ,Bujumbura.
Makabiliano ya
risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga .mwandishi wa BBC
aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa
limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa
nchi kwa sasa.
Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya
kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo
yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini
wameripotiwa kupoteza maisha.
Habari zinasemekana kwa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, aliondoka nchini Tanzania jana saa moja usiku baada ya kupatikana
taarifa za kupinduliwa kwake na kiongozi mkuu wa majeshi yake Meja
jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kwamba amempindua.
Jenerali
huyo mara baada ya tangazo lake, akaweka amri ya kufungwa kwa kiwanja
cha kimataifa cha ndege nchini humo ikiwemo mipaka ya Burundi.
Hata
hivyo haiko wazi ikiwa jeshi linamuunga mkono generali Meja jenerali
Godefroid Niyombare.
Naye msemaji wa rais wa Burundi ,amesema kwamba
wanajeshi watiifu kwa Rais ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa
viongozi nchini Tanzania,amesema nchi iko shwari.
Maelfu ya watu
wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura
baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi yake ya
kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi wakuu
wa kanda wamelaani mapinduzi hayo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi
ya watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu na
watutsi ,vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa nchini
humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa.
lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi
jirani ya Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa
na masuala ya ukabila.
Umoja wa mataifa umeonya hivi karibuni
kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa Burundi itakuwa na Amani na kama
itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo itarejea katika vita vya wenyewe kwa
wenyewe .
Via>>BBC