USHETANI!
Watoto wa kike wawili wenye umri wa miaka 8 na 14, wakazi wa Unga
Limited jijini hapa, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru baada
ya kuharibiwa vibaya sehemu zao za siri kwa madai ya kulawitiwa na
kubakwa na baba yao mzazi waliyemtaja kwa jina moja la Ezekiel.
Akizungumza
na gazeti hili kwa tabu hospitalini hapo, mtoto mwenye miaka 14
anayesoma darasa la nne, Shule ya Msingi Mkombozi (jina limehifadhiwa)
alisema alianza kubakwa siku nyingi na baba yake huyo huku siku zingine
akifanyiwa ukatili huo kwa usiku kucha huku akipata maumivu makali.
MSIKIE MWENYEWE
“Mimi na ndugu yangu
tulikuwa tukiishi na baba na wadogo zangu wengine lakini baba
alinihamishia mimi kwenye kitanda chake chumbani kwake nikawa nalala
naye na akawa ananibaka usiku na asubuhi. Jua linapochomoza nilikuwa
natoka,’’ alidai mtoto huyo.
“Nilikuwa
naumia sana. Kila nilipoona usiku unaingia moyoni nilikuwa nikisema
muda wa mateso umefika. Nilikuwa napenda kulala ili niamke kwenda shule,
lakini baba alikuwa haniachii! Hali hiyo ilinifanya kesho yake nishinde
nasinzia.”
ALIKUWA AKITUMIA VITISHO
Binti huyo aliongeza
kuwa, pamoja na kuingiwa na akili ya kutaka kuwaambia majirani, lakini
baba yake alimwendea mbele kama alijua kwani kila alipomaliza unyama
huo alimwambia angemchoma kisu kama angetoboa siri hiyo kwa watu au kwa
mama yake mzazi.
KUMBE MAMA ALIFUKUZWA
“Mtu wa kumwambia
matatizo hayo ni mama yangu mzazi ambaye baba alimfukuza nyumbani na
alikuwa akiishi sehemu nyingine. Hata hivyo, nilipomwambia mama kwamba
baba anatubaka, hasa mimi usiku kucha mpaka naamka nimechoka na siwezi
kutembea, aliniambia nisijaribu kumwambia mambo hayo ya kijinga.”
KUBAKWA KUNAENDELEA!!
Binti huyo alitoa ya moyoni kuhusu kisa chake hicho cha kubakwa na kulawitia kwa kusema:
“Sijui ni nini?! Siku
nyingine nikiwa na mdogo wangu tunayesoma naye shule, tuliitwa na babu
mmoja anaitwa Elias. Tulikwenda hadi nyumbani kwake.
“Tulipofika,
babu alitupa chipsi na kula. Halafu alimwambia mwenzangu atoke nje na
kuanza kunibaka mimi. Alipomaliza, alimuita mwenzangu, naye akambaka.
Alikuwa akitupatia chipsi kisha wakati wa kuondoka alitupa shilingi elfu
mbili (2,000).
MARA TATU ZATAJWA
Uwazi lilipomuuliza binti
mwingine wa miaka nane kuhusu kufanyiwa unyama huo, alisema: “Mimi babu
Elias alinibaka mara tatu sehemu za mbele na sehemu za nyuma, akanipa
shilingi elfu mbili na chipsi.”
MJUMBE WA MTAA AZUNGUMZA
Kwa upande wa balozi wa
eneo hilo, Janet Tirisho alipoulizwa kuhusu ukatili huo, alisema kuwa
alifanikiwa kuwaokoa watoto hao ambao walizoea kufanyiwa mchezo huo
mchafu wa kubakwa kwa muda mrefu huku mama yao akidaiwa kupokea fedha
kutoka kwa wanaye hao.Alisema sakata hilo walilifikisha Kituo Kikuu cha
Polisi Arusha na watuhumiwa wakafunguliwa jalada lenye namba
AR/RB/6252/2015- KOSA LA KUBAKA.
UCHUNGUZI WA KIDAKTARI
Daktari mmoja ambaye
hakupenda jina lake kuandikwa gazetini alisema watoto hao wamefanyiwa
uchunguzi na wamegundilika kuwa wameharibika vibaya sehemu zao za siri.
Naye
Katibu wa Afya, Hospitali ya Mount Meru, Enjo Kimati, aliyezungumza
kama msemaji wa hospitali hiyo alisema kuwa matukio ya ubakaji
yameongezeka maradufu kwani watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 15
wamekuwa wakifikishwa hosptalini hapo na kugundulika wamebakwa na
kulawitiwa.
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Arusha, SACP Leberatus Sabas (pichani) amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema: “Tumefanikiwa kumtia mbaroni babu Elias lakini
baba mzazi, Emmanuel Ezekiel alitoroka. Jeshi la polisi linamsaka ili
afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu shitaka la kubaka
linalomkabili.”
Credit: Uwazi via Gpl
Social Plugin