Maelfu
ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wameanza
mgomo kuingia darasani kwa madai ya kutopewa fedha za kujikimu kwa
zaidi ya wiki 11 huku wakitaja gharama za maisha zikiwa zimepanda mara
dufu.
Wakiongea katika viwanja vya chuo kikuu jijini Dar es Salaam kwa
kile walichokiainisha kuwa ni njaa kali pamoja na kueleza kuendelea na
mgomo hadi fedha zitakpoingia kwenye akaunti zao wametaja serikali
kuchelewesha fedha hizo kupitia bodi ya mikopo kuwa ni kuwadhoofisha
kimasomo.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof.
Rwekaza Mukandara pamoja na kukiri madai ya wanafunzi elfu saba kati ya
zaidi ya elfu kumi wanaofadhiliwa na serikali kupitia bodi ya mikopo
kucheleweshewa fedha zao kuwa ya msingi amesema tayari amezungumza na
bodi ya mikopo ambao wamemwahidi kuleta fedha zao haraka iwezekanavyo na
kuwaomba wanafunzi kurejea madarasani kuendelea na masomo.
Wakati huo huo takribani wanafunzi 400 wa chuo kikuu cha Mt. Joseph cha Mbezi jijini Dar es Salaam mwaka wa kwanza wamesimamishwa masomo
kwa muda usiojulikana baada ya kugoma kuingia madarasani wakidai fedha
za kujikim kutoka bodi ya mikopo tangu mwezi Desemba mwaka jana hadi
sasa wakieleza kuishindwa kuendesha maisha yao ya shule na kuhimili
mazingira ya kupangha nyumba mitaani.
Katika taarifa ya kusimamisha wanafunzi hao iliyotolewa na makamu
mkuu wa chuo cha Mt.Josephu Bw.Loyola Proteep aliyeambatana na mkuu wa
wanafunzi maarufu kama Dean anakiri madai ya wanafunzi hao kuwa ya
msingi na kuongeza kuwa waliwaomba utulivu na kuingia Madarasani wakati
wakifuatilia madai yao bodi ya mikopo bila ya mafanikio na uongozi
kuchukua uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza hadi
vikao vya bodi vitakapoamua vinginevyo.
Via>>ITV
Social Plugin