Matukio ya watoto kuwaua wazazi wao bado yameendelea kutoka katika maeneo mbalimbali duniani.
Sababu kubwa huenda inasababishwa na
malezi ambayo hupewa na wazazi wao hadi kupelekea kuwa na tabia aidha ya
kuwatishia maisha na wengine hufikia hatua ya kuwaua wazazi wao kwa
sababu mbalimbali.
Stori ya leo inatokea huko Japan ambapo
mtoto wa miaka 15 amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kumuua mama
yake mzazi pamoja na bibi yake ambao walimtaka kufanya kazi za shule
‘homework’ kabla ya kwenda kulala.
Mtoto huyo baada ya kufanya tukio hilo
alijipeleka mwenyewe kituo cha polisi na baada ya kufanyiwa uchunguzi
alikutwa na kisu chenye damu ndani ya begi lake na polisi walipofika
nyumbani walikuta miili ya watu hao wakiwa tayari wamefariki.
Alipohojiwa mtoto huyo alisema aliamua kufanya hivyo baada ya kukerwa na shinikizo la wazazi wake hao kumtaka kufanya homework.
Social Plugin