Mchezaji wa Stand United (Chama la Wana) Chidi Abusalimu Ebiere akishangilia gori lake la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza
Mashabiki wa Stand United (Chama la Wana) wakishangilia-Picha na Marco Maduhu |
Pichani aliyevaa shati jeupe juu ni mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akishangilia timu ya Stand United |
Pichani aliyevaa shati jeupe ni mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akishangilia timu ya Stand United |
Shabiki wa Stand United bwana Mwita akiwa amevua nguo |
Shabiki wa Stand United akionesha mbwembwe zake baada ya ushindi uwanjani |
Shabiki wa Stand akionesha mbwembwe uwanjani |
Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa uwanjani |
Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Dakika 90 za mchezo wa lala salama kati ya Ruvu Shooting na Stand United (Chama la Wana) uliofanyika katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga zimemalizika kwa timu ya Stand United kuibamiza Ruvu Shooting bao 1-0
Stand United wamejipatia goli la kwanza kupitia kwa mchezaji Mnigeria Chidi Abusalimu Ebiere dakika ya 17 kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo haya Stand United imepanda daraja, itashiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao 2015/2016 ikiwa na pointi 31.
Kutoka Shinyanga timu mbili ,Mwadui FC na Stand United zitashiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao .
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Social Plugin