Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Yereeee!! STAND UNITED YAPASUA ANGA MCHEZO WA LALA SALAMA!! YAINYUKA RUVU SHOOTING,ANGALIA PICHA MBWEMBWE ZAO UWANJANI

Shabiki wa Stand United bwana Mwita akiwa amevua nguo akishangilia timu yake -Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1
Mashabiki wa Stand United (Chama la Wana) wakishangilia timu yao katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo -Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Mchezaji wa Stand United (Chama la Wana) Chidi Abusalimu Ebiere akishangilia gori lake la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza


Mashabiki wa Stand United (Chama la Wana) wakishangilia-Picha na Marco Maduhu
Pichani aliyevaa shati jeupe juu ni mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akishangilia timu ya Stand United

Pichani aliyevaa shati jeupe ni mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele akishangilia timu ya Stand United

Shabiki wa Stand United bwana Mwita akiwa amevua nguo

Shabiki wa Stand United akionesha mbwembwe zake baada ya ushindi uwanjani

Shabiki wa Stand akionesha mbwembwe uwanjani

Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa uwanjani

Picha zote  na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Dakika 90 za mchezo wa lala salama kati ya Ruvu Shooting na Stand United (Chama la Wana) uliofanyika katika dimba la CCM Kambarage mjini Shinyanga zimemalizika kwa timu ya Stand United kuibamiza Ruvu Shooting bao 1-0

Stand United  wamejipatia goli la kwanza kupitia kwa mchezaji Mnigeria Chidi Abusalimu Ebiere dakika ya 17 kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo haya Stand United imepanda daraja, itashiriki katika ligi kuu ya Vodacom  Tanzania bara msimu ujao 2015/2016 ikiwa na pointi 31.

Kutoka Shinyanga timu mbili ,Mwadui FC na Stand United zitashiriki katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao .

Na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com