WATU sita wamekufa na wengine 45 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani zilizotokea leo na jana mkoani Singida.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka amesema leo kuwa ajali ya kwanza ilitokea Juni 11 mwaka huu saa 1.30 usiku eneo la
Manga nje kidogo ya mji huu kwenye Barabara Kuu ya Singida – Mwanza.
Alisema
ajali hiyo ililihusisha basi lenye usajili wa namba T174 CAV Scania la
Kampuni ya Nice Line linalomilikiwa na Enock Mwita wa jijini Mwanza
ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza.
Dereva
wa basi hilo aliligonga kwa nyuma gari la mizigo lenye namba za usajili
RAT 317N/ RL 0754 aina ya Benz lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa
barabara hiyo na kusababisha vifo vya abiria watatu papo hapo. Wengine
wawili walifia hospitalini na kusababisha majeruhi 37.
Kwa
mujibu wa Kamanda Sedoyeka, dereva huyo ambaye alikimbilia
kusikojulikana baada ya ajali kutokea, alikuwa kwenye mwendo kasi.
Katika ajali nyingine iliyotokea Juni 12 saa 12.15 asubuhi katika eneo
la Kindai kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma nje kidogo ya mji huu,
gari aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 998 CWG liliacha njia
na kupinduka kisha kusababisha kifo cha abiria mmoja na majeruhi
wanane.
Alisema
abiria wa gari hilo walikuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda
Kahama mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuhudhuria mazikoi ya ndugu yao na
gari lao lilipofika eneo la ajali kwenye kona kali dereva wake, Paul
Bundala alishindwa kulimudu kutokana mwendo kasi.
Baadhi
ya waliokufa katika ajali hiyo ni Shija Masanja,Yohana Chimole na
Febronia Kway. Miili ya waliotajwa na wengine watatu ambao majina yao
hayajatambuliwa imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida ambapo
pia wamelazwa majeruhi.
Social Plugin