Zaidi
ya akina mama 500 wafugaji wa kabila la kitaturu toka katika kata ya
bukundi wilayani Meatu mkoani Simiyu wameandamana hadi kwa mkuu wa wilaya hiyo
wakishinikiza kupewa miili ya vijana wao wawili waliouawa kwa kupigwa
risasi na askari wa kampuni ya Mwiba Holding iliyowekeza katika pori la
makao wilayani humo.
Akina mama hao wamefika mjini Meatu majira ya saa mbili asubuhi
wakiwa ndani ya maroli na walipofika eneo la mjini Mwanhuzi makao makuu
ya mji wa Maeatu waliteremka na baada ya muda mkuu wa wilaya hiyo Erasto Sima akiongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo aliowaomba
warudi katika kijiji cha Bukundi kwenye makao makuu ya kata hiyo ili
aweze kuongea nao lakini waligoma kata kata kurudi huko.
Baada ya viongozi wa akina mama hao kuwasihi ndipo walipokubalina
kwenda kwenye uwanja wa shule ya msingi,Mwanuhzi ambapo waliandamana
chini ya ulinzi wa polisi na walipofika hapo walianza kutoa kilio chao
cha kutaka wapewe miili ya watoto wao na kwamba iwapo mkuu wa wilaya
hatawasikiliza basi wataenda kumuona rais kwani wamechoka na manyanyaso
ya mwekezaji huyo.
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji nchini,George Bajuta ambaye pia
alikuwepo katika mkutano huo amesema wafugaji hao wamekuwa wakiishi kama
wakimbizi katika nchi yao na kwamba sasa imetosha na hawataendelea
kuvumilia kuona wafugaji wakiuwawa kwa kupigwa risasi na mwekezaji huyo.
Akijibu malalamiko ya wafugaji hao mkuu wa wilaya hiyo amesema
serikali imelishughulikia kwa kina suala hilo ikiwa ni pamoja na
kuwakamata wahusika waliofanya tukio hilo ambapo pia bado wanaendelea na
upelelezi wa tukio hilo kauli ambayo hata hivyo akina mama hao
waliipinga na kudai kuwa wa serikali ya wilaya imekuwa haiwatendei haki
bali imekuwa ikimtetea mwekezaji kampuni ya mwiba.
Mbunge wa jimbo hilo Meshaki Opurukwa ameitupia lawama serikali kwa
madai kuwa suala hilo limekuwa la muda mrefu na mwekezaji huyo amekuwa
akiuwawa wafugaji na kutochukuliwa hatua.
Aidha alimtaka mkuu wa wilaya
hiyo kutangaza kuanzia leo kusikitishwa kwa shughuli za kampuni ya Mwiba
katika pori hilo hadi muafaka wa miili ya watu hao ipatikane na pia
ofisi ya mkuu wa wilaya iwape chakula akina mama hao ambao wamegoma
kurudi majumbani hadi wapate miili hiyo kauli ambayo ilipingwa na mkuu
wa wilaya hiyo kwa madai kuwa suala hilo linashughulikiwa.
Via>>ITV
Hata hivyo hadi itv inatoka eneo la tukio hilo akina mama hao
walikuwa bado wamepiga kambi katika uwanja wa shule hiyo ambapo wamesema
kamwe hawataondoka na sasa wanajipanga kwenda kumuona rais ili
kumueleza kilio chao.
Via>>ITV
Social Plugin