ANGALIA PICHA- KILELE CHA MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO KANDA YA ZIWA (SIDO) MKOANI SHINYANGA






Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Juni 2,2015 ndiyo kilele cha maonesho ya bidhaa za viwandani kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na shirika la Viwanda Vidogo nchini SIDO.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ndiye aliyefunga maonesho hayo yaliyodumu kwa siku 5 yakihusisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Kabla ya kufunga maonesho hayo ambayo yamefanyika mkoani Shinyanga,mkuu wa mkoa huo Ally Rufunga alitembelea mabanda mbalimbali.

Malunde1 blog,ilikuwepo eneo la tukio,mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha zifuatazo.......


Mwanafunzi Asha Hamis kutoka chuo cha VETA Shinyanga akipanda kwenye mtambo unaitwa Loader na kuonesha utaalam wake wa kufanya kazi kwa kutumia mtambo huo,baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kutembelea banda la chuo cha VETA


Mwanafunzi wa chuo cha VETA akiendesha mtambo katika viwanja vya Shycom leo Juni 02,2015

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akimpongeza mwanafunzi wa VETA Asha Hamis aliyeendesha Loader na mwenzake Jafari ( katikati) aliyeendesha Greda hapo uwanjani

Mkuu wa mkoa akiwa na vijana wa VETA ambao ni wataalam wa kuendesha magreda na Loader

Hapa ni katika banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga,moto ukiwa unawaka ikiwa ni sehemu ya maonesho ya jeshi hilo,ambapo baada ya moto kuwashwa ulizimwa kisha maafisa wa jeshi hilo kuonesha njia mbalimbali za kuzima moto mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga

Moto ukiwa unawaka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizima moto huo


Maafisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga wakionesha kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa kutumia maji

Afisa wa jeshi la zimamoto mkoa wa Shinyanga akionesha jinsi ya kuzima moto akiwa juu ya gari lao

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa ameshikilia kopo la dawa za asili katika banda la wataalam wa tiba za asili,kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,nyuma yake ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku,akifuatiwa na mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede

Mkuu wa mkoa akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiulizia matumizi ya dawa ya Vidonda vya Tumbo katika moja ya mabanda ya tiba za asili

Mcheza ngoma ya Wanunguli akiwa ameshikilia mnyama fisi katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga

Fisi akiwa eneo la tukio,huku mcheza ngoma ya wanunguli akionesha mbwembwe zake mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga

Burudani inaendelea

Jukwaa kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya 13 ya viwanda vidogo kanda ya ziwa.Pamoja na mambo mengine aliwataka Wajasiriamali nchini kuzingatia ubora wanazozalisha ili kuingia katika soko la ushindani wa bidhaa zao na kuongeza ufanisi wa bidhaa zao.

Rufunga aliwataka watanzania kuthamini bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali nchini kwani ni bora na zenye kiwango kinachotakiwa.Baada ya kutoa hotuba ya kufunga maonesho hayo,mkuu huyo wa mkoa alitoa vyeti kwa washiriki pamoja na zawadi kwa wajasiriamali walifanya vizuri katika maonesho hayo

Wajasiriamali kutoka Shinyanga wakiwa eneo la tukio

MC akiendelea kutoa miongozo mbalimbali

Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi akizungumza wakati wa kufunga maonesho hayo ambalo aliwaomba wajasiriamali kuacha kufanya biashara kwa mazoea na waendelee kuzalisha bidhaa zenye ubora kama walivyoonesha katika viwanja vya Shycom.

Picha ya pamoja -baadhi ya washiriki wa maonesho hayo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga

Maonesho hayo ya Viwanda Vidogo kanda ya ziwa yaliyoanza kufanyika mkoani Shinyanga tarehe 28 mwezi Mei na yamemalizika yakishirikisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania na kauli mbiu ya mwaka huu inasema; “Buni, Boresha, Jifunze biashara kupitia SIDO.”

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post