Picha>>MHESHIMIWA BENARD MEMBE APOKELEWA KWA SHANGWE SHINYANGA,APATA WADHAMINI 683,AWAPUUZA WATIA NIA YA URAIS
Friday, June 19, 2015
Hapa katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini ambapo leo Waziri
wa mambo ya nje ya nchi mheshimiwa Benard Membe aliyetia nia kuwania urais katika uchaguzi
mkuu ujao,amefika kuchukua majina ya wadhamini wake wanaomuunga mkono katika harakati za kuelekea Ikulu-Pichani ni wanachama wa CCM wakiimba na kucheza wakati wa kumpkea mheshimiwa Benard Membe.Malunde1 blog huwa haipitwi na matukio,ilijisogeza eneo la tukio kujua kilichokuwa kinajiri,Mwandishi wetu Kadama Malunde,ametulelea picha zifutazo
Mheshimiwa Benard Membe akiwasilia katika ukumbi wa mkutano katika ofisi za wilaya ya Shinyanga mjini
Wakazi wa Shinyanga wakiwemo wadhamini wa mtia nia huyo wakiwa ukumbini
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga ambaye
pia mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida akizungumza katika ukumbi wa ofisi
za CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakati mheshimiwa Benard Membe akichukua
majina ya wadhamini wake 683 kutoka mkoa wa Shinyanga.Mheshimiwa Mayenga Mtia
nia ya urais Benard Membe ni muadilifu hivyo anaweza kuoingoza nchi ya
Tanzania.
Mbunge
wajimbo la Mchinga mkoa wa Lindi Said
Mtanga akieleza kumuunga mkono Benard Membe katika harakati zake za kuwania
urais Tanzania.
Katibu
wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza katika ukumbi huo wakati wa kukabidhi fomu na kadi za wadhamini waliojitokeza kumdhamini mtia nia ya urais Benard Membe
Tunafuatilia kinachojiri.....
Katibu
wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akikabidhi fomu ya majina ya
wadhamini 683 kwa mheshimiwa Benard Membe.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini kanali mstaafu Tajiri Maulid akimkaribisha mheshimiwa Benard Membe,ambapo alisema mtia nia huyo ana sifa za kuwa rais wa Tanzania.
Mheshimiwa Benard Membe akizungumza katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo alisema kuna watu wamechukua fomu kugombea nafasi ya urais lakini ukiangalia nafasi waliyoomba ni kubwa kuliko uwezo wao bora wangeomba kugombea nafasi zingine zinazolingana nao kuliko kuleta utani, kwenye nafasi hiyo nyeti
Membe aliwataka watanzania kuacha kushabikia watangaza nia wasio kuwa na sifa za kuongoza nchi wanaopita katika mikoa mbalimbali kwani nafasi ya urais ni nyeti haihitaji watu wasio na uwezo.
Mheshimiwa Membe akizungumza ambapo alisema bado anaamini CCM bado ni chama bora kuliko vyote nchini,hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuiangusha CCM lakini changamoto ni mamluki wanaoharibu chama hicho kwa kujiona wao ndiyo wao katika chama.
Askofu wa kanisa la Emmanuel mjini Shinyanga Edson Mwombeki (katikati) akifuatilia kwa umakini hotuba ya mheshimiwa Benard Membe
Wakazi wa Shinyanga wakishikana mkono na mheshimiwa Benard Membe baada ya kumaliza hotuba yake
Wakazi wa Shinyanga wakishuhudia kilichokuwa kinaendelea kwenye ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin