ANGALIA PICHA_ JINSI MTANGAZA NIA YA URAIS MKULIMA WA DARASA LA 7 ALIVYOWASILI SHINYANGA KUCHUKUA WADHAMINI WAKE
Sunday, June 21, 2015
Hapa ni katika ofisi za Chama Chama Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini.Pichani katikati ni mtangaza nia kuwania urais nchini Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kupitia CCM,Lidephonce Bilohe,ambaye ni mkulima mwenye elimu aya darasa la saba akisaini fomu ya majina ya wadhamini 30 aliopata katika mkoa wa Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Bilohe ambaye ni mkulima amesema amekaa muda mrefu katika
chama akitamani kuwa rais wa nchi na matarajio yake ni ushindi kutokana na
uwezo na uzoefu wake ndani ya chama pamoja na kwamba elimu yake ni darasa la
saba.
Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni Naibu
waziri ofisi ya makamu wa rais Mazingira,akizungumza katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo pamoja na mambo mengine alimtakia kila kheri mtangaza nia huyo ndugu Bilohe katika harakati zake za kusaka urais
Mheshimiwa Stephen Masele akishikana mkono na mtangaza nia kuwania urais nchini Tanzania kupitia CCM Lidephonce Bilohe
Lidephonce Bilohe amepata wadhamini 30 kutoka mkoa wa Shinyanga na kuwaahidi watanzania
kumuunga mkono kwani anayo nia dhabiti ya kuwaongoza wananchi.
Mtangaza nia Lidephonce Bilohe akiwapungia,ambaye anafanya ziara ya kusaka wadhamini peke yake, mkono wakazi wa Shinyanga nje ya ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini leo.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin