**************
Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,
Makongoro Nyerere, leo amerejesha fomu ya kugombea urais kupitia Chama Cha
Mapinduzi(CCM) baada ya kumaliza zoezi la kukusanya saini za wadhamini.
Makongoro ambaye jana alihitimisha zoezi la kukusanya saini
za wadhamini mkoani Shinyanga, amekusanya saini za wadhamini katika mikoa yote
30 ya Tanzania.
Akizungumza na Malunde1 blog , Makongoro amesema
amemaliza hatua ya kwanza ya safari yake ya kuwania kwenda Ikulu hivyo hatua ya
pili anamuachia Mwenyezi Mungu kuiangazia safari yake ya kwenda Ikulu.
“Nimemaliza zoezi la kukusanya saini za wadhamini nchi
nzima…leo nimereshesha fomu zangu kwa ajili ya kusubiri utaratibu mwingine wa
kichama, hatua hii mwenyezi Mungu ndiye anajua muelekeo wangu wa mbio hizi"-Makongoro
ANGALIA PICHA HAPA CHINI WAKATI MAKONGORO AKIKABIDHI FOMU LEO
Social Plugin