MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri
wa Mawio na Mwanahalisi online ,Edson
Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa Juni 29 mkoani Kagera.
Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio
na Mwanahalisi online ,Edson
Kamukara wamesema ni pigo kwa tasnia ya
habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya
uandishi wa habari .
Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara
ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.
“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi
kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa
wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbowe
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi
amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia
misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
“Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri
kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema
Mengi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama
hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson
Kamukara katika viwanja vya Leaders Club
Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki
(katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama
hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson
Kamukara katika viwanja vya Leaders Club
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Hali
Halisi Publisher wachapishaji wa Mawio na Mwanahalisi Online,Sued Kubenea
wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana
mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ,Freeman Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa
Mawio ,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri
wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja
vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waombolezaji wa kuaga mwili wa Mhariri wa Mawio
,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akitoa
hishima za mwisho wakati wa kuaga Mwili
wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara
katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akitoa hishima
za mwisho wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri
wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja
vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media
wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari wakiwa katika huzuni wakati
wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es
Salaam.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya
Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club
Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki
dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba
mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT),
Regnald Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson
Kamukara. Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa
utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati),
akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa
marehemu
Wanahabari ni huzuni na vilio
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati
wa kuuaga mwili wa Edoson Kamukara.
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya
Majengo, Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya
sh.500,000.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa
mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa
mikataba ya ajira kwa wanahabari.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT),
Regnald Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said
Kubenea alikuwa akifanya kazi na marehemu Edson Kamukara.
Ni vilio tu kwa wanahabari.
Shughuli ya uagaji ikiendelea.
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.
Safari ya kuelekea Kagera kwa ajili ya maziko ya Mwili wa Mhariri wa Mawio
,Edson Kamukara katika viwanja vya
Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)
(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)