Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MAMIA WAJITOKEZA KUAGA MWILI WA MWANDISHI WA HABARI EDSON KAMUKARA

MAMIA wamejitokeza katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online  ,Edson Kamukara aliyefariki mwishoni wiki na anatarajiwa kuzikwa  Juni 29 mkoani Kagera.
Wakizungumza wakati wa kuaga kwa aliyekuwa Mhariri wa Mawio na Mwanahalisi online  ,Edson Kamukara  wamesema ni pigo kwa tasnia ya habari kutokana na kuwa na kusimamia kitu anachoamini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari .

Akizungumza juu ya kifo chake ,Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema kifo cha kamukara ni pigo kutokana na kuwa na msimamo wa bila kuyumbusha na bahasha.
“ Ni bora kuishi kwa kusimama kwa muda mrefu kuliko kuishi kwa kupiga magoti kwa muda mfupi hiyo ikiwa ni kuangalia kutumia kalamu kwa wanyonge bila masilahi ya wanasiasa”amesema Mbowe 
 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP.Reginard Mengi amesema Kamukara alikuwa jasiri katika kufanya mbambo yake kwa kusimamia misingi ya habari na alikuwa hangalii fedha.
“Fedha angekuwa Kamukara anaiangalia basi angekuwa tajiri kwani alikuwa ni mtu kusimamia misingi ya habari kwa ajili ya wanyonge”amesema Mengi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Freeman  Mbowe akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Hamis Kagasheki (katikati)akiwa na viongozi wa Chadema ,Kushoto ni  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Freeman  Mbowe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho,Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) ,Freeman  Mbowe akiteta jambo na Mkurugenzi wa Hali Halisi Publisher wachapishaji wa Mawio na Mwanahalisi Online,Sued Kubenea wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akipeana mkono Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema) ,Freeman  Mbowe wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginard Mengi wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waombolezaji wa kuaga mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Reginard Mengi akitoa hishima za mwisho  wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chadema ,Dk Wilbroad Slaa akitoa hishima za mwisho  wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na Sayari wakiwa katika huzuni wakati wa kuaga Mwili wa Mhariri wa Mawio, Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.
 
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Kamukara wakati ulipowasili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi, kwa ajili ya kuagwa. Kamukara alifariki dunia juzi na mazishi yake yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi (katikati), akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk.Wilibrod Slaa kwenye uagaji wa mwili wa Edson Kamukara. Kulia ni Mbunge wa Bukoba mjini, Khamis Kagasheki.
Mmoja wa waandishi wa habari akiwa amepoteza fahamu wakati wa kuaga mwili huo.
Wanahabari na waombolezaji wengine wakiwa wamejipanga foleni wakati wa utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edson Kamukara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea (katikati), akisaidiwa baada ya kuishiwa nguvu wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu
Wanahabari ni huzuni na vilio
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki wakati wa kuuaga mwili wa Edoson Kamukara.
Wanafamilia ya marehemu wakiwa kwenye shughuli hiyo
Sehemu ya umati wa watu katika shughuli hiyo.
Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma na marehemu Shule ya Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi akizungumza kabla ya kutoa rambirambi yao ya sh.500,000.
Viongozi wa serikali na vyama vya siasa wakiwa kwenye shughuli hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika uagaji wa mwili wa marehemu ambapo alipigania waajiri wa vyombo vya habari kutoa mikataba ya ajira kwa wanahabari.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Regnald Mengi akimfariji Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea alikuwa akifanya kazi na marehemu Edson Kamukara.
Ni vilio tu kwa wanahabari.
Shughuli ya uagaji ikiendelea.
Dada ya marehemu Edson Kamukara akitoa heshima za mwisho.

Safari ya kuelekea Kagera kwa ajili ya maziko ya  Mwili wa Mhariri wa Mawio ,Edson Kamukara  katika viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.


(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com