Askofu Msaidizi wa
Kanisa la la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya
Mashariki na Pwani, Chediel Lwiza (kushoto) akitoa ibada fupi ya
kumwombea marehemu.
MAKAMU wa Rais, Dk.
Gharib Bilal, jana aliongoza mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Ukonga, Eugene Mwaiposa, huko Ukonga Kipunguni ‘A’ Matembele jijini Dar
es Salaam ambako simanzi na vilio vilitawala miongoni mwa umati
uliohudhuria huko akiwemo Waziri wa Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia;
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda.
Katikati ni mume wa marehemu, Ally Mwaiposa, mtoto wao Salimila Mwaiposa (kushoto) na Mektrida Mwaiposa (kulia).
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Mecky Sadick (kushoto), Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib
Bilal (katikati) na Anne Makinda wakiwa katika maombolezo.
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akisalimia waombolezaji
wakati alipofika nyumbani wa marehemu Eugene jana.
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa msibani.
Social Plugin