Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, akiingia ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro Dar es Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mke wake Ester Frederick Sumaye kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania nafasi ya urais wakati ukifika iwapo jina lake litapitishwa na chama chake cha CCM.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akiwa na mke wake
Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (kulia), akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (katikati), akiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kiluvya, Juma Semendu Nauchiwa. Kada wa CCM, Shabani Uronu, Mama Ester Sumaye na Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Kaenja.
Mwanahabari Ibrahim Yamola akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.
Mwanahabari Mariam Mziwanda akimuuliza swali Waziri mstaafu Sumaye baada ya kutangaza nia ya nafasi hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Msanii Oscar Nyerere akitoa burudani katika mkutano huo.
Wananchi wakimpongeza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye baada ya kuzungumza nao.
Msanii Shafii Omari akitoa burudani.
Makada wa CCM na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye ametangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar leo.
Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia akiwa Dar es Salaam maana anataka kuwatumikia Watanzania wote siyo wa nyumbani kwake pekee.
Kauli mbiu yake ni ‘Uongozi Bora, Komesha Rushwa, Jenga Uchumi’.
Kiongozi huyo amesema ametangaza nia baada ya kujipima, akajitafakari na kujiridhisha kuwa anatosha kuwania nafasi hiyo.
Sumaye amesema dira ya taifa katika miaka 10 ijayo ni kwamba Tanzania ifikie uchumi wa kati.
Aidha kiongozi huyo ametumia muda huo kuelezea kiongozi anayetakiwa na Watanzania kuwa:
-Kwanza ajipime, ajitafakari na ajiridhishe kuwa anatosha nafasi hiyo
-Ajipime kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira
-Mzalendo, anayejua tulipotoka na tunapotaka kufika
-Kiongozi ambaye ni mtumishi atakayewatumikia wananchi na si bosi
-Kiongozi anayefikiri na kushauriwa
-Kiongozi anayeweka maslahi ya Tanzania mbele na si yake binafsi
-Kiongozi atakayelinda amani ya Tanzania na Muungano wake.
-Mwenye uwezo wa kusimamia uchumi
-Atakayeboresha huduma za jamii zisizobagua watu.
-Atakayesimamia elimu ya Tanzania kurejea ilipokuwa hapo awali na kuiendeleza zaidi
-Atakayepambana na rushwa, ujangili na madawa ya kulevya.
Mhe. Sumaye pia amewatupia swali baadhi ya makada wa CCM waliotangaza nia na kudai kuwa wanauchukia umasikini hivyo kuamua kuutafuta utajiri Ikulu ambapo amewataka kama wanataka utajiri upo mitaani waende wafungue makampuni.
(Habari wa Hisani ya Global Publishers).