Heka heka imetokea Shinyanga
ambapo Bibi mmoja kaachiwa nyumba na marehemu mume wake, lakini masharti
yake hataki mpangaji wake ajifungulie nyumbani kwake na wala hataki
mtoto mchanga nyumbani kwake.
Akisimulia mkasa huo mmoja wa wapangaji
wake ambaye alifikiwa na mtoto huku bibi huyo bila huruma akimzuia
kuingia ndani ya nyumba yake kwa ajili ya taratibu za mazishi alisema
amesikitishwa sana na kitendo hicho kwa kuwa si cha kibinadamu.
Alisema aliopanga kwa bibi huyo tangu
mwaka 2013 na alipewa masharti ya kutokuwa na watoto na hata alipobeba
mimba alikwenda kujifunguliwa kwao na kukaa kwanza hadi mtoto alipokuwa
mkubwa kidogo kisha kurejea ingawa bibi huyo hakutaka arudi na mtoto
wake.
Mtoto huyo aliugua gafla na kufariki
dunia lakini cha kushangaza bibi huyo alimfukuza na kukataa maiti
kuingizwa nyumbani kwake hivyo kuwalazimu kupeleka msiba kwa Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa Rashid Abdalah alisema wapangaji
wengi wamekua wakimlalamikia bibi huyo kwa kuwafukuza wanapokuwa
wajawazito na alidai marehemu mume wake aliweka zindiko ndani ya nyumba
hiyo.
Kitendo cha bibi huyo kiliwakasirisha
watu ambao walijazana nyumbani kwake kutaka kujua sababu ya yeye kufanya
hivyo, lakini bibi huyo alionekana kuwa na jazba huku akiwafukuza na
kutotaka kuwasikiliza.
Hekaheka iko hapa, utasikia wahusika wote wakisimulia mkasa ulivyokuwa.
Social Plugin