Mufti Shekh Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba enzi za uhai wake |
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba amefariki dunia leo katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam. Akithibisha kutokea kwa kifo hicho, Kaimu Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Mh Mary Nagu amesema msiba huo umetokea leo asubuhi na kwamba marehemu alikuwa akisumbulia na kisukari na shinikizo la moyo kwa muda mrefu. Mh. Nagu amesema serikali inaungana na waislamu wote kuomboleza msiba huo, na kumuelezea marehemu kwamba alikuwa ni kiungo muhimu kati ya waislamu na serikali.
Baraza la Waisilamu
Tanzania BAKWATA limesema kesho mwili wa marehemu utaagwa jijini Dar es salam na mazishi yatafanyika siku ya Alhamis mkoani Shinyanga.
#RIPShabanSimba Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajiun | ||
Social Plugin