Vitambulisho viwili tofauti vya kijana huyo
Mkazi
wa Kijiji cha Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga Kefa Eriabu
(27)ambaye ni wakala wa mabasi, amekamawata na Jeshi la Polisi kwa kosa
la kujiandikisha mara mbili kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
kinyume na sheria.
Tukio
hilo limetoka leo majira ya saa mbili kamili asubuhi baada ya Mtuhumiwa
huyo kutoa vitambulisho hivyo kwa lengo la kuwaonesha wenzake kwamba
amefanikiwa kujiandikisha mara Mbili.
Hata hivyo baada ya
wenzaka kuona hali hiyo walimhoji kwa nini amejiandikisha zaidi ya mara
moja na baadaye walitoa taarifa kwa jeshi la Polisi katika kituo cha
Isaka ambao walifika na Kumkamata kwa mahojianao zaidi.
Kijana
huyo alijiandikisha kwa mara ya kwanza 18/6,2015 katika kituo cha Isaka
Stationi kwa jina la “Kefa D Eriabu kuzaliwa 01/01/1988 na kupewa kadi
No T-1004-7969-449-9.
Aidha alifanya hivyo siku ya jumamosi
20/06/2015 katika kituo cha Shule ya Msingi Isaka, wa jina la Kefa D
Jonhson amezaliwa 10/05/1995 na kupewa kadi no,T-1004-4564-460-3.
Kijana huyo ambapo alikiri
kufanya hivyo kwa lengo la kuhofia kupoteza kitambulisho na wala hakuna
aliyemtuma kufanya hivyo.
“Ni kweli mimejiandikisha mara
mbili ila sikujua kama ni kosa, nilifanya hivyo kwa hofu ya kupoteza
kitambulisho na ndio maana nilifika kazini nikawaeleza wenzangu sijui
ilikuwa ni mtego”alisema Kefa.
Hili ni tukio la kwanza
kutokea katika wilaya ya Kahama, na ni siku tatu tangu kijana mwingine
akamwatwe mkoani Mbeya kwa kosa kama hilo.
Jeshi la Polisi wilayani Kahama linamshikilia kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamiliaka atafikishwa mahakamani
Social Plugin