Huko mjini Bagamoyo katika eneo lijukanalo kwa jina la Majani Mapana kumetokea taharuki kubwa baada ya habari kuenea kuwa kuna mwanamama aliyetambulika kwa jina moja la Bi. Hatujuani aliyethibitishwa kuwa umauti umekuta, kafufuka baada ya kuthibitishwa na madaktari kuwa amefariki.
Bi. Hatujuani aliugua kwa muda na kukimbizwa hospitali ya wilaya Bagamoyo na baadaye kudhaniwa kuwa ama amepatwa na umauti baada ya kuugua malaria lakini hospitalini hapo walithibitisha kuwa ameshafariki dunia.
Mkasa huo ulitokea tarehe 28 Juni 2015 na wanandugu walishachukua maiti na matayarisho ya maziko yakiwa mbioni, turubai lilishafungwa,sanda tayari hadi Juni 29, 2015 wakimuosha maiti Bi. Hatujuani mwenye umri wa miaka 30, waliokuwa wakimuosha walishtuka maiti kuwa ana joto kali, anatoka jasho na anakunja na kukunjua mikono na miguu, lakini kusema wala kusimama hawezi wakaamua kutimua mbio!
Baada ya wanandugu kutangazia umma kuwa msiba hakuna tena bali tuna mgonjwa mahututi, waliofika msibani na umati wa watu waligoma kuondoka mazikoni hadi kieleweke nini kilichozua mtihani huu tena katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Timu ya Malunde1 blog ilifunga safari hadi
Bagamoyo na kukuta umati wa watu katika nyumba ambayo marehemu alikua
akiishi ikiwa ni muda mchache baada ya mwili wake kurejea kutoka
hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo ndipo alipofariki.
Majirani walidai baada ya mwili wa
marehemu huyo kurudishwa nyumbani ili kuanza taratibu za mazishi
walishangaa kuona bado mwili wa moto na alikuwa akijitingisha wakati
waoshaji wakimuandaa kwa ajili ya kumzika.
Majirani hao walisema waoshaji waliamua kutimua mbio baada ya kuona marehemu bado wa moto na kuzua taharuki hiyo iliyowaacha watu wengi midomo wazi.
Shangazi wa marehemu alisema ni kweli
baada ya kumleta walishangaa mwili ukiwa wa moto na mapigo ya moyo
yakifanya kazi kama kawaida licha ya madaktari kuthibitisha kuwa
amefariki, na wakaamua kusimamisha shughuli za mazishi hadi kesho yake
walipoona amekuwa wa baridi na tayari alishafariki.
Daktari aliyethibitisha kama marehemu
amefariki alisema baada ya kumpima marehemu alikuwa amefariki na kuruhusu
taratibu ziendelee, na alisema kuwa mwili wa marehemu kuwa wa moto
inategemee na mazingira ya sehemu alipohifadhiwa.
Baada ya madaktari kuthibitisha kwa mara ya pili kuwa bi Hatujuani kafariki,taratibu za mazishi ziliendelea..
Baada ya madaktari kuthibitisha kwa mara ya pili kuwa bi Hatujuani kafariki,taratibu za mazishi ziliendelea..
Na Mwandishi maalum wa Malunde1 blog- Bagamoyo