Nimekutana na stori hii kutoka Zimbabwe inamhusu Nabii mmoja kutoka nchi hiyo kufariki akiwa kwenye mishemishe za kupata nguvu za ziada ili akemee mapepo.
Nabii huyo Shamiso Kanyama alifuatwa
na familia moja wakamuomba aje nyumbani kwao ili afanye maombezi
kuondoa mapepo yaliyokuwepo kwenye nyumba ya wanafamilia hao.
Nabii huyo akaenda kufanya maombezi na
wanafamilia hao… Wakiwa katika maombezi hayo, nabii huyo alidai kuwa
roho mtakatifu amezugumza nae na kuwaomba wanafamilia hao kuchimba
kaburi nje ya nyumba ili wamzike akiwa hai, alafu akifufuka atakuwa na
nguvu mpya ya kuendelea na maombezi hayo.
Wanafamilia hao wamekamatwa na wameshitakiwa kwa kosa la mauaji.
Social Plugin