Wananchi wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamelazimika kuzima moto katika soko kuu la mji wa Masasi kwa saa nane kwa kutumia mchanga na maji baada ya kukosekana kwa gari la zimamoto.
Soko hilo linawafanyabiashara zaidi ya elfu mbili na linategemewa na wilaya za Nanyumbu na Nachingwea, wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya waathirika wamesema moto huo ulizuka majira ya saa nne usiku, na serikali haikuweza kusaidia lolote na hapa wanafafanua.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Masasi Bernad Luta ambaye alitembelea soko hilo ameiagiza kamati ya maafa ya wilaya kufanya tathimini haraka ili kubaini hasara iliyopatikana, huku akikiri wilaya hiyo kwa sasa haina gari la zimamoto.
Mbali na viongozi wa serikali waliotembelea soko hilo pia viongozi wa kisiasa kikiwemo chama cha mapinduzi, Chadema na mwenyekiti wa ACT Zitto Zuberi Kabwe ambaye yuko wilayani Masasi amewatembelea wafanyabishara na kuwapa pole.
Via>>ITV