Ripoti
ya jana Alhamis ilionyesha idadi ya watu 96 kupoteza maisha kutokana na
ajali ya moto iliyotokea katika kituo cha mafuta katika mji mkuu wa
Accra Ghana.
Hii ni idadi ya vifo ambayo imeonyesha kuongeza ambapo mpaka sasa watu waliofariki wamefikia 175 kutokana na ajali hiyo.
Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku
wakati wakazi wa mji huo walipokuwaeneo hilo wakijikinga na mvua kubwa
ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na kukosekana kwa umeme
kwa muda mrefu.
Serikali ya Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Social Plugin