Sophia Mashala( 29) mkazi wa kijiji cha Kishapu wilayani Kishapu aliyenyofolewa pua na mdomo na fisi anayedaiwa kuwa ni wa kishirikina |
Sophia Mashala( 29) akiongea kwa tabu kutokana na mdomo na pua yake kuliwa na fisi
Makovu mbalimbali aliyoyapata Sophia baada ya kuvamiwa na fisi harusini |
Hujafa Hujaumbika! Unaweza ukawa mzima leo kesho tukasikia
mengine.Sophia Mashala( 29) mkazi wa
kijiji cha Kishapu wilayani Kishapu amekuwa katika mateso kwa miaka mitano sasa
baada ya kujeruhiwa vibaya na Fisi akiwa kwenye sherehe ya mtoto wa Shemeji
yake iliyokuwa inafanyika katika kitongoji cha Nyalusanga kijiji cha Kishapu kisha
kunyofolewa pua.
Sophia anasema siku ya tukio akiwa kwenye harusi na wenzake
zaidi ya 30 tarehe 16, Oktoba 2011,siku
ya Jumamosi majira ya saa 12 jioni,ghafla
alijitokeza fisi na kumvamia yeye tu kisha kumshambulia sehemu mbalimbali za
mwili wake huku mdomo na pua yake vikinyofolewa.
Anahitaji msaada wa shilingi milioni 2 na laki tano ili
afanyiwe upasuaji kwani sasa Anapumulia mdomoni,anakauka koo,mafua yanatokea
mdomoni na kusumbuliwa na vichomi.
Tangu kutokea kwa tukio hilo la fisi anayedaiwa kuwa wa kichawi ametelekezwa na mume wake wa
ndoa Solomoni Dilu aliyezaa naye watoto wawili ambaye sasa ameamua kuoa mke
mwingine huku vitu vyote aliyevyochuma
naye akinyang’anywa na kutojali hata watoto wake.
Sophia anasema awali aliolewa kwa mahari ya ng’ombe zaidi ya
15 baada ya kupata matatizo hayo wakwe
zake walimtenga huku wakikataa kutoa pesa za
matibabu kwa madai atamaliza mahari aliyotolewa hivyo atafute sehemu
nyingine atakapopata pesa za matibabu.
Sophia amezunguka katika
hospitali mbalimbali nchini kutafuta matibabu wakati huo huo kutafuta haki
katika vyombo vya sheria lakini anadai hakuna mafanikio yoyote aliyopata kutokana
na kesi yake kupigwa kalenda kila kukicha mahakamani.
Kutoa
ni moyo,wasiliana na Sophia kwa simu
namba 0768 718 846 au 0719 213 460
MSIKILIZE HAPA AKISIMULIA JINSI ALIVYOPATA TUKIO NA
KINACHOMSUMBUA HIVI SASA
Social Plugin