Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JE ? UNAWEZA KUISHI UKIWA UCHI? KUTANA NA WATU HAWA WA AJABU DUNIANI WANAISHI UCHI KABISA

null
Watalii walio uchi wakipanda mlima
Mwandishi Mark Haskel Smith 
null
Mtalii


Watu wengi wasingejihisi vyema kuvua nguo zao zote na kusalia uchi wa mnyama katika maeneo ya uma,lakini kwa wengine ni maisha yao.

Mwandishi kutoka nchini Marekani Mark Haskel Smith alikabiliana na changamoto zote na kuweza kuishi bila nguo.

Iwapo upo katika uwanja wa ndege ,huwezi kufanya masihara kuhusu bomu.

Na iwapo uko na watu walio uchi huwezi kufanya masihara kuhusu matiti.

Na mungu wangu,usisisimkwe,utaamrishwa uondoke anasema Haskell Smith.

Haya ni mambo mawili aliyogundua alipotembelea maeneo ya kupumzika ya watu walio uchi duniani.

Ziara yake ya kwanza ilikuwa katika mgahawa wa Desert Sun Resort huko Palm Springs Carlifonia.


'Nilishtuka'.'Nilikuwa na wasiwasi katika chumba changu cha hoteli,nikijipaka mafuta baada ya mafuta hadi nilipotoka nje,nilikuwa niking'ara sana'',.


''Kuna watu chungu nzima katika kidimbwi cha maji waliokuwa ndani ya kidimbwi kimoja cha maji walioniangalia na kujifunika nyuso zao.


Nilijihisi vibaya sana,nilifikiri watu hawa wamenipita na zaidi ya miaka 20 lakini nilipojiangalia chini ''ooh mungu wangu''.


Baada ya kuzuru eneo hilo alizuru maeneo mengine ya watu walio uchi barani Ulaya.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com