KANYE WEST AMEKUJA NA UBUNIFU MWINGINE WA VIATU VINAITWA "YEEZY 350 BOOST" BEI LAKI 4
Saturday, June 20, 2015
Miaka michache iliopita Kanye West alitengeneza headlines kubwa alipotangaza kujivua ubia na Nike
kampuni maarufu ya kutengeneza viatu baada ya malalamiko kutoka kwa
msanii huyo kua kampuni hio haimlipi hela yoyote kwa ubunifu wowote
anaoutuoa katika kubuni viatu vyake chini ya kampuni ya hio.
Na mwaka 2013 Disemba Kanye West akaamua kuingia mkataba na ubia na kampuni nyingine kubwa Adidas na safari hii kwa malipo.
Chini ya AdidasKanye West aliachia kiatu chake kwanza Yeezy 750 Boost, kiatu kilicho ingia na kuisha sokoni baada ya masaa machache. Kanye West bado anaendelea kutumia fursa yake chini ya Adidas.
Safari hii Kanye hadondoshi album mpya bali anaachia kiatu chake kipya; Yeezy 350 Boost mwezi huu tarehe 27.
Kanye West alitangaza ujio wa kiatu hicho katika Press Conference ya Adidas Jumatano wiki hii, na kuahidi kuwa safari hii viatu hivyo vitapatikana
kiuraisi na kuuzwa kwa bei nafuu kidogo kuliko toleo la kwanza lilokuwa
linauzwa kwa dola $350 ambayo ni sawa na Tzs 770,000/=. Toleo la pili litapatikana sokoni kwa dola $200 sawa na Tzs 440,000/=.
Nimekusogezea baadhi ya picha za viatu hivyo hapa chini unaweza kuvitazma mtu wangu.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin