Daktari wa upasuaji nchini Afrika
Kusini amethibitisha kwamba mwanamme wa kwanza aliyepandikizwa uume
atakuwa baba hivi karibuni.
Professor Andre van der Merwe, ambaye
ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba, amesema mwenza
wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi minne.
Mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anafanyiwa tohara ambayo haikufanikiwa.
Professor
van der Merwe ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa
upandikizwaji huo wa kiungo umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa
wagonjwa wengine katika siku zijazo.
Via>>BBC
Social Plugin