KUHUSU TUKIO KUBWA NA LA KIHISTORIA WIKI HII SHINYANGA



Katika kile ambacho naweza kusema haijawahi kutokea,taasisi ya Mzalendo Foundation nchini isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na masuala ya Utawala Bora,Haki za binadamu,utamaduni na michezo imeandaa mchezo wa Hisani kati ya wakongwe wa soka  Simba na Yanga  Veterani utakaofanyika Alhamis Wiki hii,kwa ajili ya kutafuta pesa kusaidia watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino) katika kituo cha Buhangija kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
 -Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog


Mwenyekiti wa Mzalendo Foundation Khamis Mgeja akizungumza katika na waandishi wa habari ambapo taasisi yake inalaani vitendo vya kukatili dhidi ya albino yanayoendelea na kuongeza kuwa wameamua kuandaa mchezo huo wa hisani wa magwiji wa soka nchini kwa ajili ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasadia watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wanaoishi maisha magumu wakikabiliwa na changamoto nyingi kubwa zaidi ikiwa ni Chakula.
Mgeja mesema katika mchezo huo wa hisani,hapatakuwa na kiingilio chochote bali,mtu mwenye mapenzi mema na watoto hao,atatakiwa kuja na mchango wa angalau kuanzia shilingi 1000/= tu na kuendelea kama sehemu ya mchango kwa mahitaji ya watoto hao wanaokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo chakula
,magodoro,vyandarua,vitanda,mavazi na mafuta maalumu kwa walemavu wa ngozi.

Mgeja ametaka wabunge kuipigia kelele ili kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto wenye ulemavu ambao wanahitaji msaada ili kunusuru maisha yao huku akizitaka hamshauri za wilaya zinazopeleka watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija kutoa msaada badala kutelekeza watoto hao katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga pekee.Pia aliiomba serikali kuona umuhimu wa kutenga bajeti kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
Taasisi hiyo ya Mzalendo Foundation ni taasisi ya kwanza nchini kuandaa mchezo wa hisani kwa ajili ya kusaidia watoto hao,ambapo mgeni rasmi siku hiyo atakuwa mtu mkubwa sana/mtu mwenye heshima zaidi
Katibu wa taasisi ya Mzalendo Foundation  Shaban Nguno akizungumzia changamoto zinazokikabili kituo cha Walemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona cha Buhangija ambapo alisema hivi sasa watoto hao wanahitaji chakula,magodoro 100,shuka 800,vyandarua 400,vitanda 70,mavazi zikiwemo nguo za ndani,mafuta ya kujipaka (mafuta maalumu kwa albino) hivyo kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza Juni 11,2015 kuleta chochote walichonacho

Mkutano unaendelea

Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Benester Lugola akizungumza ambapo amesema wanashirikiana na Taasisi hiyo ili kufanikisha lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu wa ngozi katika kituo hicho ambao maisha yao ni magumu hivyo kuwaomba wananchi kujitokeza katika mchezo huo.

Meneja wa Uwanja wa CCM Kambarage Meja mstaafu Mohamed Ndaro amesema wanaendelea kufanya marekebisho katika uwanja huo na kufikia Juni 10,2015 uwanja utakuwa tayari kwa matumizi.

Mjumbe wa Mzalendo Foundation ndugu Emmanuel Nzungu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kuwa mstari wa mbele kusaidia makundi ya watu wasiojiweza hivyo kuwaomba kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi yao kuwasaidia watu wenye mahitaji wakiwemo watoto na wazee

Mjumbe wa Mzalendo Foundation Alhaji Alei Juma akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kuwa wazalendo wa kujitolea kwani ni aibu kubwa kusikia kuwa watoto hao wamekosa msaada

Mjumbe wa Mzalendo Foundation Alhaji Alei Juma alitumia fursa hiyo kuwataka watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya albino kuacha tabia hiyo kwani haimpendezi hata mwenyezi mungu hivyo kuwataka watanzania kuishi kwa upendo.
Kituo cha watoto wenye ulemavu cha Buhangija hivi sasa kina jumla ya watoto 396 kati yao albino 292,wasiiona 40 na wasiosikia 64 na kutokana na ongezeko la albino kwa hofu ya kuuawa changamoto kubwa ni chakula.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post