KUHUSU TUKIO KUBWA NA LA KIHISTORIA WIKI HII SHINYANGA
الاثنين, يونيو 08, 2015
Katika kile ambacho naweza kusema haijawahi kutokea,taasisi
ya Mzalendo Foundation nchini isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na masuala
ya Utawala Bora,Haki za binadamu,utamaduni na michezo imeandaa mchezo wa Hisani
kati ya wakongwe wa soka Simba na Yanga Veterani utakaofanyika Alhamis Wiki hii,kwa ajili ya kutafuta pesa kusaidia
watoto wenye ulemavu wa ngozi(albino) katika kituo cha Buhangija kilichopo
katika manispaa ya Shinyanga.
-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Mzalendo Foundation Khamis Mgeja akizungumza
katika na waandishi wa habari ambapo taasisi yake inalaani vitendo vya kukatili dhidi ya albino yanayoendelea na kuongeza kuwa wameamua kuandaa mchezo huo wa hisani wa
magwiji wa soka nchini kwa ajili ya kutafuta pesa kwa ajili ya kuwasadia watoto
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wanaoishi maisha magumu wakikabiliwa na
changamoto nyingi kubwa zaidi ikiwa ni Chakula.
Mgeja mesema
katika mchezo huo wa hisani,hapatakuwa na kiingilio chochote bali,mtu mwenye
mapenzi mema na watoto hao,atatakiwa kuja na mchango wa angalau kuanzia
shilingi 1000/= tu na kuendelea kama sehemu ya mchango kwa mahitaji ya watoto
hao wanaokabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo chakula
,magodoro,vyandarua,vitanda,mavazi na mafuta maalumu kwa
walemavu wa ngozi.
Mgeja ametaka wabunge kuipigia kelele ili kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto wenye ulemavu ambao wanahitaji msaada ili kunusuru maisha yao huku akizitaka hamshauri za wilaya zinazopeleka watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija kutoa msaada badala kutelekeza watoto hao katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga pekee.Pia aliiomba serikali kuona umuhimu wa kutenga bajeti kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
Taasisi hiyo ya Mzalendo Foundation ni taasisi ya kwanza nchini kuandaa mchezo wa hisani kwa ajili ya kusaidia watoto hao,ambapo mgeni rasmi siku hiyo atakuwa mtu mkubwa sana/mtu mwenye heshima zaidi
Katibu wa taasisi ya Mzalendo Foundation Shaban Nguno akizungumzia changamoto zinazokikabili kituo cha Walemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona cha Buhangija ambapo alisema hivi sasa watoto hao wanahitaji chakula,magodoro 100,shuka 800,vyandarua 400,vitanda 70,mavazi zikiwemo nguo za ndani,mafuta ya kujipaka (mafuta maalumu kwa albino) hivyo kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza Juni 11,2015 kuleta chochote walichonacho
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti
wa Chama Cha Soka mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Benester Lugola akizungumza ambapo amesema
wanashirikiana na Taasisi hiyo ili kufanikisha lengo la kusaidia watoto wenye
ulemavu wa ngozi katika kituo hicho ambao maisha yao ni magumu hivyo kuwaomba
wananchi kujitokeza katika mchezo huo.
Meneja
wa Uwanja wa CCM Kambarage Meja mstaafu Mohamed Ndaro amesema wanaendelea
kufanya marekebisho katika uwanja huo na kufikia Juni 10,2015 uwanja utakuwa
tayari kwa matumizi.
Mjumbe wa Mzalendo Foundation ndugu Emmanuel Nzungu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kuwa mstari wa mbele kusaidia makundi ya watu wasiojiweza hivyo kuwaomba kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi yao kuwasaidia watu wenye mahitaji wakiwemo watoto na wazee
Mjumbe wa Mzalendo Foundation Alhaji Alei Juma akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kuwa wazalendo wa kujitolea kwani ni aibu kubwa kusikia kuwa watoto hao wamekosa msaada
Mjumbe wa Mzalendo Foundation Alhaji Alei Juma alitumia fursa hiyo kuwataka watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili dhidi ya albino kuacha tabia hiyo kwani haimpendezi hata mwenyezi mungu hivyo kuwataka watanzania kuishi kwa upendo.
Kituo cha watoto wenye ulemavu cha Buhangija hivi sasa kina
jumla ya watoto 396 kati yao albino 292,wasiiona 40 na wasiosikia 64 na
kutokana na ongezeko la albino kwa hofu ya kuuawa changamoto kubwa ni chakula.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin