Wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Uingereza wamezindua mipira ya kiume ‘kondomu’ yenye uwezo wa kugundua maradhi ya zinaa wakati watumiaji wanapokutana kimwili.
Kondomu hiyo inayojulikana kama S.T.EYE inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria waliopo kwa muhusika.
Kutukana na kuvumbua mipira hiyo wanafunzi hao tayari wametunukiwa tuzo ya ubunifu na kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia ya ‘the TeenTech’ pamoja na pauni 1,000.
Wanafunzi hao wamesema wameamua kufanya
hivyo kwa lengo la kusaidia vizazi vijavyo ili kuepukana na maradhi
yanayoweza kuzuilika kitaalam.
Social Plugin