Tokyo ni moja kati ya miji maarufu inayofahamika kwa kuwa na huduma ya karibia kila hitaji la mwanadamu duniani, unaweza usiamini ila Tokyo iliyopo ndani Japan ni nchi inayoongoza kwa kuwa na kila huduma inayokidhi mahitaji ya kimapenzi duniani kitu ambacho kinaweza kukufanya uione Japan kama ni walevi wa mapenzi.
Lakini fikra hizi zinaweza zikabadilisha mtazamo wako kuhusu nchi hii pale utakapokutana na Takashai Sakai mwanaume mwenye miaka 41 ambaye hajawahi kukutana na mwanamke toka azaliwe.
Akiwa katika miaka ya 40 na zaidi
mwanaume huyu hajawahi kabisa kukutana na mwanamke, kushikana mikono
wala kumkumbatia mwanamke yoyote.
Lakini Takashai hayuko peke yake nchini Japan, kwani utafiti unaonyesha kwamba moja kati ya wanaume wanne wakijapan kwenye rika la miaka 30 hadi 40 hawajawahi katika maisha yao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, kushiriki tendo la ndoa wala kuoa!
baadhi wakiwa wameanua kuishi maisha ya namna hiyo ila kwa wengi waliopo
hali hii haikuwa chaguo lao bali walijikuta tuu hawawezi, na wangependa
hali hii ibadilike kwani wanatamani kuonja ulimwengu huo sasa.
Lakini kwa asilimia kubwa ya wanaume wenye hali hii Japan darasa la uchoraji wa watu wakiwa hawajavaa nguo ambalo linaitwa “Nude Art Class”
.. hili ni suluhisho dogo kwa uhalisia walio nao na kwa upande wa pili
ni fursa pekee walionayo kumuona mwanamke akiwa mtupu!! Mmoja ya walimu
wa vipindi hivyo alisikika kwenye interview fupi akisema;
>>> “madarasa
kama haya hujaribu kuwasaidia watu kama hawa kuenjoy uumbaji wa jinsia
ya kike kupitia uchoraji, tunafanya hivi kuijenga saikolojia ya wanaume
hawa kuwaona wanawake sio watu wa kuwaogopa na hatimaye kuvunja uwoga
wao wa kufanya mapenzi, hii ndio dhamira yetu”.
Watafiti wamesema ongezeko la wanaume
wenye shida hii imekua ikionekana kama kikwazo kwa ukuwaji wa nchi
kwasabau idadi ya wanaume hawa inavyo ongezeka, idadi ya uzaaji
unapungua na hatimae kupunguza idadi ya watu nchini. Hili linaoneka kua
kama janga kwa moja ya nchi yenye uchumi mkubwa duniani.