Hizi stori ziko nyingi sana zinazohusu
wazazi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watoto wao, wako wanaoenda mbali
zaidi na kufanya ukatili kama wa kubaka na kulawiti watoto pia.
Imenifikia hii kutoka Zimbabwe, baba
kambaka mtoto wake na kwenye kujitetea anasema kwamba eti ni utaratibu
na utamaduni wao kutembea na mtoto wa kwanza ndani ya familia.
Polisi hawakumwachia, mzee huyo
amefunguliwa mashtaka kwa kosa la ubakaji lakini bado alichoendelea
kujitetea ni maneno yake yaleyale kwamba huo ni utamaduni wao kabisa !!
Wazazi wa mtoto huyo walitengana, siku
ya tukio binti aliamua kwenda kumsalimia baba yake… baba huyo akavamia
ndani ya chumba cha mtoto huyo na kumbaka.
Social Plugin