Edward Lowasa ameendelea kuvunja rekodi ya idadi ya watu wanaojitokeza kumdhamnini baada ya kupata wadhamini 120,392 jana mkoani Arusha.
Rekodi hiyo ya Arusha imezipiku ile iliyowekwa na mkoa ya Iringa alikodhaminiwa na wanachama 58,562.
Mbunge
huyo wa Monduli aliwasili jijini Arusha saa 9:00 alasiri na kupokelewa
kwa mbwembwe zilizoambatana na nyimbo mbalimbali za wasanii kadhaa
nchini. Lowassa aliongozana na mkewe Regina na viongozi kadhaa wa CCM.
Mara
baada ya kuwasili uwanjani hapo, Lowassa alifanyiwa maombi rasmi na
wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai, maarufu kama Malwaigwana.
Katibu
mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isaack Joseph alisema waliomdhamini
waziri huyo mkuu wa zamani ni wanachama hai kutoka wilaya zote saba za
kichama mkoani Arusha.
Social Plugin