Matumizi
ya mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram ni kitu
ambacho kimeshika chati sana kwa sasa duniani, vijana wameonekana kuwa
waathirika wakubwa wa matumizi ya mitandao hii.
Kijana
Little Wang ambaye umri wake ni miaka 19 huko China aliona njia pekee
ya kukomesha tabia yake ya kupenda kutumia laptop na simu kuingia
mtandaoni ni kujikata mkono wake, alipoona hali haimwendei sawa aliita
taxi impeleke Hospitali ambapo hakuna aliyejua kinachoendelea nyumbani
kwao, aliacha ujumbe kwamba ametoka kwenda Hospitali na angerudi muda
mfupi baadaye.
Madaktari walimfanyia operation kuunga mkono huo huku wakiwa na matumaini kwamba baadae utaweza kufanya kazi kama ilivyokuwa mara ya kwanza kabla hajaukata.
Madaktari walimfanyia operation kuunga mkono huo huku wakiwa na matumaini kwamba baadae utaweza kufanya kazi kama ilivyokuwa mara ya kwanza kabla hajaukata.
Mama yake Little alisononeshwa na kitendo hiki na kusema hakutegemea mtoto wake angeweza kujifanyia ukatili wa aina hii.
Social Plugin