Wanawake katika kijiji kimoja cha
kaskazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na
mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea
kwa takribani miaka 10.
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa
serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji
cha Apaa huko Amuru.
Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia
ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku wakazi wakidai kwamba ardhi hiyo
ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika
kabila la Acholi ,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya
kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake.