Pata picha unaingia zako supermarket,
unanunua mahitaji mbalimbali ya jikoni na unabaki na hesabu moja tu
nyepesi kwamba ukifika home kazi yako ni kupika, alafu unakuja
kufungua unakutana na vitu vya ajabu.
Muhammad Hussain na mkewe Sanam wanaishi Birmingham, Uingereza.. Walitoka
zao Supermarket na vitu mbalimbali walivyonunua, kuja kuingia jikoni
kwa ajili ya kuandaa chakula mwanamke huyo akakuta ndani ya kopo la
nyanya kuna mjusi aliyekufa.
Pamoja na kupeleka malalamiko yao kwa uongozi wa Supermarket hiyo inayoitwa Masala Bazaar
waliombwa radhi kwa kitendo kilichotokea, wakaahidiwa kwamba
kutafanyika uchunguzi jinsi gani imetokea mpaka mjusi huyo kaingia ndani
ya kopo hilo ambalo ni ka nyanya ambazo zimesindikwa toka Italy.
“Mke wangu
alikuwa jikoni anaandaa chakula cha mchana, nikasikia anapiga kelele..
kwenda nikakuta ndani ya kopo hilo la nyanya kuna mjusi aliyekufa“– Muhammad Hussain.
Social Plugin