Mwanamke mmoja nchini Nigeria ametangaza kupitia redio kuwa anatafuta
mume, akisema atampa gari na nyumba. Mamia ya wanaume walifurika kituo
cha radio cha Freedom, mjini Kano ambapo
polisi walilazimika kuitwa kutuliza watu. Msichana huyo, Zainab
Abdulmalik, 22, amesema alikuwa amekasirishwa mno na 'boyfriend' wake wa
zamani.
Mtangazaji wa redio - Nasiru Zango- ameiambia BBC kuwa Zainab
alichagua mchumba kutoka katika mlolongo mrefu wa wanaume waliokuwa
wamejipanga nje ya kituo cha redio na kuondoka.
Social Plugin