Wakati
chama cha waandishi wa habari wanawake(TAMWA) kikilaani ukatili katika
jamii mwanamke mmoja mkazi wa Sokoine Road mjini Songea mkoani Ruvuma
Bi.Rehema Gwaya amefanyiwa ukatili na mke mwenzake kwa kumwagiwa mafuta
ya moto usoni na kuungua sehemu mbalimbali za mwili wake.
Bi. Rehema Gwaya ambaye amelazwa katika Hospitali ya mkoa Songea
akiwa na mwanae wa miezi saba anasema chanzo cha kufanyiwa ukatili huo
ni kutofautiana na mke mwenzake aitwaye Zefania Chimgege baada ya kuhoji
masuala ya usafi ambapo Zefania aliyekuwa akipika maandazi akamwagia
karai la mafuta ya moto usoni.
Baada ya kufanyiwa unyama huo shemeji yake ambaye ni mume wa
Zefania Bw.Hafidh Hamidu Mbaya akamwambia atoke nje ammalizie kwa
kumchoma na kisu.
Mganga mfawidhi katika hospitali ya mkoa Songea(HOMSO) Dkt.Benedikt
Ngaiza amesema amempokea mgonjwa huyo
Wakazi wa Songea wamelaani
ukatili huo.
Rehema Gwaya na Zefania Chimgege wameolewa sehemu moja na wote
wanaishi katika nyumba ya baba Mkwe na waume zao na kwamba Zefania Chimgege anashikiliwa na polisi kwa kufanya ukatili huo.
Via>>ITV
Via>>ITV
Social Plugin