ANGALIA PICHA_ WANANCHI WAGOMBANIA KUMZIKA MUFTI SIMBA MJINI SHINYANGA
Wednesday, June 17, 2015
Katika hali ambayo iliyotafsiriwa kuwa shehe mkuu wa
Tanzania Mufti Issa Shaaban bin Simba alikuwa kipenzi cha watu,jana wakati wa mazishi
yake,maelfu ya wakazi ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga walijitokeza
kumsindikiza mpendwa wao katika nyumba yake ya milele katika makaburi ya
Waislam ya Nguzo nane mjini Shinyanga.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida waombolezaji walijipanga
kuanzia nyumbani kwa marehemu mtaa wa Majengo hadi kwenye makaburi ya Nguzo
Nane mjini wakisubiri kubeba mwili wa marehemu mufti Simba.
Mbali na maelfu ya watu kufurika nyumbani kwa marehemu mtaa
wa Majengo,pembezoni mwa barabara,wakazi wa Shinyanga waligombania kuingia
katika makaburi ya Nguzo nane pamoja na kwamba askari wengi wa jeshi la polisi
walitanda eneo hilo kuimarisha ulinzi.
Wakazi wa Shinyanga walilazimika kusukumana na polisi huku
wengine wakilazimika kupanda juu ya miti ili kuona kilichokuwa kinaendelea
wakati wa mazishi hayo.Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
ANGALIA PICHA HAPA CHINI UONE HALI ILIVYOKUWA
Wananchi wakisaidia na polisi kuzuia wananchi wasiingie katika makaburi ya Nguzo nane kwani nafasi ilikuwa haitoshi
Wakazi wa Shinyanga wakiwa wamening'inia kwenye ukuta unaozunguka makaburi ya Nguzo nane
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane,wengine waliambuliwa kupanda kwenye miti na ukuta uliopo katika makaburi hayo
Kaburi la Mufti Simba
Msafara wa rais Jakaya Kikwete aliyeongoza mazishi ya mufti Simba ukiondoka makaburini,huku wakazi wa Shinyanga wakiwa pembezoni mwa barabara karibu na soko la Nguzo nane
Social Plugin