MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AMTOSA LOWASSA SAKATA LA URAIS TANZANIA
Wednesday, June 17, 2015
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, Stephen Masele (kulia) akisalimiana
na Naibu waziri wa fedha nchini, Mwigulu Nchemba muda mfupi mara baada
ya (Nchemba) kuwasili katika ofisi za CCM Shinyanga mjini, wakati
Nchemba alipokuwa akitafuta wanachama wa CCM wa kumdhamini. Kulia
mwanzoni ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya siasa, Rajabu Abasi -Picha na
Suleiman Abeid
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini, Stephen
Masele ametoa ufafanuzi kuhusiana na madaiya kumuunga mkono mmoja wa
makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaowaniakugombea urais kwa tiketi
ya CCM na kukanusha habari zilizoandikwa nabaadhi ya vyombo vya habari
vilivyodai amejiunga kwenye kambi ya MheshimiwaEdward
Lowassa.
Masele ambaye pia ni Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Mazingira) alitoaufafanuzi huo juzi alipokuwa akimkaribisha kada
mwingine wa CCM, MwiguluNchemba aliyefika katika ofisi za CCM Shinyanga
mjini kwa ajili ya kutafutawana CCM wa kumdhamini ili aweze kuteuliwa
kugombea urais kwa tiketi ya CCM.
AkifafanuaMasele alisema yeye kama
mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ni wajibu wake pamojana viongozi
wengine wa CCM wilayani humo kuhakikisha wanamsaidia kada ye yotewa
chama anayekwenda kwa ajili ya kutafuta wadhamini na hakuna mtu
anayemuunga mkono miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais kwa
vile wote ni wake.
“Sisi kama wajumbe wa kamati ya siasa ni wajibu
wetu kuandaa mazingira mazuri kwa watangaza nia wetu na makada wenzetu
wote wanaokuja katika eneo letu hili, na mimi kama mbunge ninao wajibu
kabisa wa kushiriki kikamilifu kuhakikisha kwamba mambo yote yanakuwa
sawasawa, nawapongeza wale wote mliojitokeza kumdhamini pia
mwenzetuMwigulu Nchemba,”.
“Sisi huku wengine siyo wajumbe wa NEC na
walasiyo wajumbe wa Kamati kuu, lakini ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM
Taifa, kazi yetuni kusubiri vikao vya juu vya chama vifanye kazi yake
na hatimae vitatuletea mgombea wa CCM na tutapigana kufa na kupona
kuhakikisha chama chetu kinashinda,”alieleza Masele.
Kwa upande wake
kada wa CCM na Naibu waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza na
wanachama wa CCM 45 waliojitokeza kumdhamini wakiwemo wazee maarufu wa
mjini Shinyanga alisema moja ya lengo lake kuu la kutaka kugombea nafasi
ya urais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwavusha watanzania kuelekea katika taifa lenye uchumi wa kati.
Mwigulu alisema anaamini
mgombea wa CCM ndiye atakayeibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu
wa Oktoba 25, mwaka huu na kwamba wanachosubiri watanzania walio wengi
hivi sasa ni kuona chama chake kinampa ridhaa ya kupeperusha bendera
yaCCM ili waweze kumchagua.
“Vyanzo vyangu vya habari na taarifa
mbalimbali zinaonesha watanzania wengi wanasubiri chama changu kinipe
ridhaa ya kupeperusha bendera ili wao waweze kuunga mkono agenda yao
waliyoiona tangu nilipotangaza nia ya kugombea urais, sina mashaka ndani
ya chama na nje ya chama kwamba agenda ya watanzania ikishindanishwa na
jambo lolote itashinda tu,”
“Kwa wana CCM, CCM inapata uhalali wa
kuongoza taifa letu kwa aina tatu ikiwemokutoka urithi wa vyama
vilivyokomboa taifa letu, pili kwa kazi ilizozifanya kwakuunda serikali
tangu ilipoanzishwa mpaka hivi sasa na kazi zakuliletea taifa hili
maendeleo tangu ilipoanzishwa mpaka hivi leo, na pia sifa yatatu ni
kwa kazi inazotarajia kwenda kuzifanya sasa,” alieleza
Nchemba.
Aidha kada huyo wa CCM alirejea kauli zake za awali kwa kueleza
kuwa moja ya agenda yakekuu atakapofanikiwa kuingia Ikulu ni kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya kipato chakati pamoja na watanzania wenyewe kuwa
watu wa nchi ya kipato cha kati na waondokane na kauli ambayo wameisikia
muda mrefu ya uchumi kukua huku wao wakiona umasikini ndiyo
unaokua.
Katika hatua nyingine Mwigulu alikanusha madai kwamba kitendo
cha kujitokeza idadikubwa ya makada wa CCM kutaka kuteuliwa kugombea
urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa ni chanzo ya chama hicho
kusambaratika baada ya majina yamakada wengi kukatwa wasiweze kugombea
nafasi hiyo.
“Si kweli kwamba eti CCM itasambaratika mara baada ya uteuzi
wa mgombea wake katikanafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano, tupo
imara na tutaendelea kuongoza nchihii, hatuwezi kusambaratika, maana
watanzania hawataangalia sura ya mtu,wataangalia agenda kuu watakayoisimamia ili kuifanya nchi kuwa ya uchumi wakati,” alieleza
Nchemba.
Aidha alitoa wito kwa wana CCM katika dua zao zote kuhakikisha
wanatafuta mgombea waCCM anayetokana na CCM na siyo yule mgombea
aliyepitia CCM na kwamba yeye mwenyewe anaamini amejitokeza katika wakati
sahihi na kwa mahitaji sahihi yawatanzania na kwamba anaamini
akichaguliwa kuwa rais atawavusha.
Na Suleimna Abeid-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin