Kesi za wanawake kushindwa kutambua muda wao wa kujifungua unapofika
zimekuwa zikitokea mara kwa mara na hata wengine kushindwa kujitambua
kama ni wajawazito hadi pale unapokaribia wakati wa kujifungua.
Kuna hii nyingine imetokea kule China ambapo mwanamke mmoja amejikuta
akijifungua njiani bila kujua wakati anakwenda hospitali baada ya
kusikia uchungu.
Qi aliongozana na mumewe Li wakitumia usafiri wa pikipiki kwenda hospitali ya Chenguang Nongchang kwa
ajili ya kujifungua lakini kwa bahati mbaya mama huyo alijifungua
njiani bila kutambua na mtoto kubakia barabarani ikiwa ni maili mbili
kabla ya kufika hospitalini hapo.
Baada ya kufika hospitali na madaktari kumcheki walikuta tayari mtoto
ametoka huku mama huyo akitokwa damu na baada ya kufanya uchunguzi
iligundulika mama huyo amejifungua njiani akiwa njiani bila kujua na
mtoto wake kuokolewa na watu wengine.
Mama huyo akiongozana na madaktari walirudi kuangalia ni wapi mtoto
huyo amedondoka na kumkuta akiwa amezungukwa na watu bila kuwa jeraha
lolote na kumkimbiza hospitali ili kufanyiwa uchunguzi wa kina juu ya
afya yake.
Social Plugin