Akiuguzwa na mke wake aliyemsababishia kujeruhiwa na mgoni wake.
Riego
Solo (28), mkazi wa Mbezi ya Tangi Bovu, Dar es Salaam anadaiwa
kuchomwa kisu kwenye koromeo katika jaribio la kuchinjwa na mgoni wake
aliyejulikana kwa jina moja la Jacob akiwa katika harakati za kumzengea
mkewe.
Tukio hilo la kinyume na kawaida ya wanaofumania kufanya uhalifu, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Mbezi ya Tangi Bovu.
Taarifa
zilizopatikana katika eneo la tukio zinadai kwamba, Solo alivamiwa na
mgoni wake huyo hatua chache toka nyumbani kwake ambapo wananchi
walimsaidia baada ya kupiga kelele na walipofika eneo la
Uwazi baada ya kupata taarifa hizo, lilimfuata Solo nyumbani kwake akiwa ametoka Hospitali ya Mwananyamala, Dar alikolazwa.
Mwanaume huyo alikiri kufanyiwa jaribio la uchinjwaji shingoni na mgoni wake huyo. Alisema:
“Siku
hiyo nilikuwa nimetoka kazini. Nilipofika nyumbani, sikukuta chakula,
mke wangu alikuwa hajapika. Nikaamua kwenda kununua chakula mahali
lakini karibu na hapa kwangu.
“Nikiwa
njiani saa mbili usiku, nilivamiwa na mtu. Alinipiga kwanza kabla ya
kuniwekea kisu shingoni, akanijeruhi. Lakini nilimwangalia vizuri
nilimjua kuwa ni mgoni wangu, Jacob.
“Tulipambana
naye, nikamzidi nguvu lakini tayari alishanijeruhi kwa kunichinja
shingoni. Alikimbia huku akiniacha nikigaragara chini. Nilipiga kelele
kuomba msaada. Naamini alikuwa na lengo la kuniua ili amrithi mke wangu
lakini Mungu ni mkubwa bado nipo hai.
“Huyu
Jacob, kuna wakati niliwahi kumuonya kuhusu mke wangu aachane naye,
aliniambia amemuacha, hatarudia tena kutembea naye. Lakini cha
kushangaza bado akawa anamnyemelea na amekuwa akijificha karibu na hapa
kwangu. Watu ndiyo huwa wananiambia, sasa amenijeruhi.
“Kwa
kweli Mungu mkubwa, aliyeniokoa wa kwanza ni dada mmoja anayenifahamu,
alinikuta nikigaragara chini naye akapiga kelele. Watu walikuja na
kunichukua hadi Kituo cha Polisi Kawe na kuchukua PF3 kwa ajili ya
matibabu, nikapelekwa Hospitali ya Mwananyamala.
“Nilishonwa
nyuzi kadhaa na kuwekewa ‘dripu’, baadaye niliruhusiwa kurudi nyumbani
lakini hali yangu ilibadilika ikabidi nirudishwe tena Hospitali ya TMS.
Kwa sasa mke wangu aliyetaka kusababisha nipoteze uhai ndiye huyu
anayeniuguza, bado nampenda, sitamwachia.”
chanzo: gazeti la uwazi
Social Plugin