Rehema
Chalamila aka Ray C amejikuta akishindwa kujizuia kulia baada ya
kunyimwa dawa ya Methadone ambayo amekuwa akiitumia kwa miaka miwili
sasa ili kumsaidia kuondokana na addiction ya madawa ya kulevya.
Ray C amepost video kwenye Instagram ambazo kwa zinaendelea kusambaa kwenye mtandao huo akilia kwa uchungu.
“Nashindwa
kuvumilia,” anasikika akisema. “Mpaka sasa nipo hapa kitengo cha madawa
na sijapewa dawa, kwa sababu nilipost ile post nyingine wamenifanyia
makusudi. Sasa mimi nikikosa madawa wanataka nirudi kwenye kuvuta unga,”
amehoji muimbaji huyo.
Ray
C aliendelea kudai kuwa mwili unamuuma pamoja na mifupa huku akishindwa
kujua afanye nini ili kukabiliana na hali hiyo ambayo amedai inamtesa.
Social Plugin