Rais
Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin
Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika Juni 27, 2015
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Sakata
la Mbunge wa jimbo la Geita Marehemu Donald Kelvin Max kuzikwa jijini
Dar Es Salaam pasipo wananchi wake kupata fursa ya kuaga mwili wake
limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wakazi wa jimbo la Geita
Wilayani Geita,wakiwemo baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kukana
kufiwa na mbunge wao kwa kile walichodai alikuwa mwakilishi wa eneo
alikozikwa huku chama cha mapinduzi mkoa wa Geita kikidai hakuna kanuni
zinazolazimisha mbunge kuzikwa kwenye jimbo lake.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Malunde1 blog,ikiwa ni siku moja tangu mbunge wao
kuzikwa,baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wananchi huku
wakionekana kukerwa na jambo hilo walidai kuwa,wanachojua mbunge wao
yuko hai na iwapo angekuwa amefariki dunia angeletwa Geita kuagwa na
wananchi wake.
Neema
Steven Chozaile mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita alidai
kuwa,kitendo kilichofanywa na chama cha mapinduzi cha kuruhusu mbunge wa
Geita kuzikwa kimya kimya jijini Dar kimewafumbua macho wananchi na
kwamba safari hii hawatafanya makosa katika kuchagua mwakilishi wao.
‘’Tumepata
fundisho kwamba tunapochagua mtu tuwe makini,tunayemtambua
alipozaliwa,ni mtoto wa Fulani maana haiwezekani mbunge wa Geita
asiletwe hapa akaagwa na waliomchagua tena kwa kura nyingi,kama CCM
wanaruka na helkopita kuhudhuria sherehe za mtia nia Monduli walishindwa
kutumia usafiri huo kuleta maiti ya mbunge wetu akaagwa hapa kisha
wakamzika watakapo,ndiyo maana tunasema huyo hakuwa mbunge wetu bali wa
Dar alikozikwa’’alisema.
‘’Mwaka
2010 niliamka alfajiri kwa ajili ya kuwahi foleni ili nimchague mbunge
wangu Max,nikafanikiwa..nilivyosikia kwamba amekufa sikuamini ikanibidi
nianze kutafuta msiba ulipo hadi mtaa wa Katoma wanakodai ni nyumbani
kwake’’
‘’Lakini
hakukuwa na dalili za msiba zaidi ya mikusanyiko ya wanaojiandikisha
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR,lakini wakati
nikiendelea kuhangaika nijue msiba ulipo ndiyo nilipoelezwa msiba uko
Dar na atazikwa huko..hii imetudhalilisha sana wakazi wa Geita’’alisema
Fidelis Kanani mkazi wa Nyerere Road.
Zephania
Mussa ambaye ni mkazi wa mtaa wa Nyanza Kalangalala mjini Geita,alisema
‘’Sisi Geita walishatudharau maana watu wa kuja ndiyo wanachukuwa
uongozi,mfano marehemu Max alitudanganya ni mkazi wa Geita,tutamchagua
tena nkwa kishindo tukiamini ni mwenzetu’’
‘’Kitendo
cha mbunge wetu kuzikwa nje ya hapa na bila kuagwa na waliomchagua
kimetuuma sana na huu ndiyo mwisho kwa wanaGeita kuendelea kuwa shamba
la bibi,kwa sasa mtu atakayekuja kutuomba ridhaa ya kutuongoza tutamtaka
atupeleke nyumbani kwao,tujuwe ukoo wake na mpaka alipozikwa babu yake
maana tulkijipanga tumzike mbunge wetu kwa heshima zote kumbe anazikwa
Dar imeumiza sana nasoi tunasema waliomzika ndiyo waliomchagua wetu
hajafa bado’’alisema Mussa.
‘’Sisi
kam wanageita hili jambo limetuchanganya na ndiyo maana tunasema
hatujafiwa na mbunge wafiwa ni wakazi wa Dar,haiwezekani mtu
tuliyemwamini kama mwakilishi wetu azikwe kimyakimya sisi tuliopigwa
mabomu ajili yake tusimuage na kwa nini azikwe huko,inamaana
alitudanganya ni mkazi wa Geita ili hali sivyo?’’alihoji Lucas Charles
mkazi wa mtaa wa Moringe.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita Kamanda Alphonce Mawazo
akitoa maoni yake alisema‘’Maoni yangu ni kwamba tumehadaiwa,mimi
nilitoka mbeya kumzika mbunge wangu nikiwa sina shaka atazikwa
Geita,kumbe tulichagua tulichagua mtalii na ndiyo maana alitelekeza
jimbo kwa muda mrefu akiwa hajaanza kuugua maradhi yanayomsumbua’’
‘’Mbunge
ni lazima awe na uhusiano wa ardhi ya pale anapowakilisha,awe na
wajomba,dada,shangazi,babu zake, watu aliocheza nao utotoni,aliosoma
nao,angalu awe anaguswa na damu ya pale,lakini sisi wana Geita tulichagua kwa ushabiki na hatukujua kwamba tulichagua mtalii’’
‘’Msiba huu umetufumbua macho na umetufundisha mambo mengi kwamba
inatubidi tutambue kwamba Ubunge ni Uchifu na Chifu hawezi kutoka eneo
jingine,lazima atoke eneo lilelile alilozaliwa maana kama mimi
nilitegemea niwape pole ndugu zake,mama,mke wake na ndiyo maana nikatoka
Mbeya kuwahi mazishi harafu nikakuta hata harufu ya msiba hakuna’’
‘’Kwa kweli wana Geita tumejisikia vibaya na sisi wananchi tujifunzekwani na maendeleo hayaji kwa kuchagua mtu asiye mkazi,kwani angekuwa mkazi ningempa mkono wa pole shangazi yake lakini hakuwepo,nimekuja Dar napo sikufanikiwa maana sikujua hata msiba uko wapi’’alisema Mawazo.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,Joseph Kasheku Musukuma alipotakiwa
kuzungumzia hali hiyo alidai kuwa,maiti ni ya familia ya Max na hakuna
kanuni kwenye chama chao cha Mapinduzi(CCM)zinazowalazimishwa azikwe
eneo alilokuwa akiliwakilisha kama Mbunge.
‘’Anayehoji
kwa nini Mbunge wao hakuzikwa Geita,mwambie kuwa maiti siyo ya ccm ni
ya familia ambayo ndiyo ilitoa ratiba ya wapi azikwe,mi sidhani kama
kuna sababu ya yeye kuzikwa Geita wakati kwao ni Dar es Salaam na ndugu
zake wengine wamezikwa huko,kama wanasema walimchagua kwa kishindo na
wanashangaa kuona hakuzikwa Geita waulize wakati anaumwa nani
aliyekwenda kumsalimia kwa kishindo?’’alisema Musukuma
Mbunge Max alifariki juni 23 katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuwa amelazwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi(ICU)kwa zaidi ya mwaka mmoja akisumbuliwa na kansa ya
Ubongo kwa zaidi ya miaka mitatu ambapo alipatiwa matibabu nchini India
kabla ya kurudishwa hapa nchini. Alikuwa mbunge wa jimbo la Geita tangu
mwaka 2010 hadi mauti yanamkuta na amezikwa juni 27,2015 makaburi ya
Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Na Victor Bariety-Malunde1 blog Geita