Watu
wawili wamejeruhiwa na zaidi ya kaya 78 zimeezuliwa na mvua
iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kijiji cha Kasoto
wilayani Geita.
Mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa nane mchana kukatika baada
ya masaa matatu imeezua paa na nyumba 17 kubomoa kabisa hivyo kukosa
kabisa mahali pa kuishi.
Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Omary Mangochie ametembelea kijijini
hapo na kujione uharibifu wa majengo na kumtaka mhandisi wa wilaya ya
Geita kufanya tahimini ya uharibifu uliuojitokeza, aidha amewataka
baadhi ya wananchi kuwasaidia wale waliopatwa na maafa.
Social Plugin