Kila mmoja anatambua kuwa elimu haina mwisho na kadri miaka inavyokwenda watu wengi wamekuwa wakitambua nini maana ya elimu huku wengi wao wakiamua kurudi darasani ili kujiongezea ujuzi zaidi.
Unamkumbuka yule kikongwe wa miaka 90 Priscilla Gogo huko Kenya aliyekuwa akisoma darasa la tano na wajuu zake wapatao sita? aliaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi duniani kusoma shule ya msingi.
Priscilla Gogo
Ukiachia stori hiyo wiki chache zilizopita huko Ujerumani kikongwe wa miaka 102 alihitimu PHD yake ya udaktari, Leo tena nimekusogezea ya bibi huyu Doreetha Daniel aliyeamua kuudhihirishia uma duniani baada ya kumaliza shahada yake kwenye chuo cha Canyons huko Santa Clarita, Carlifonia.
Akiwa na miaka yake 99 alianza kuisaka safari yake ya elimu mwaka 2009 na kupania kupata degree yake kabla ya kutimiza miaka 100.
Bibi huyo amevunja rekodi katika chuo hicho kwakuwa mwanafunzi mzee zaidi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho miaka 45 iliyopita.