Hali sio nzuri Afghanistan, kingine
kilichochukua headlines kwenye TV za Kimataifa na Mitandaoni ni ishu ya
kuvamiwa kwa Bunge la nchi hiyo, mabomu na risasi vimetumika pia !!
Wavamiaji hawakuwa na nia njema, ripoti zinaonesha jamaa hao walikuwa sita na ni members wa Kundi la Taliban.
Polisi wamefanikiwa kuwaua jamaa hao
ambao walikuwa na silaha pamoja na mabomu, hapa ninazo picha ambazo
zinaonesha jengo la Bunge kwa ndani likiwa na moshi mzito.
Wavamiaji hao walilipua gari moja nje ya Jengo la Bunge kabla ya kuvamia ndani !! Watu 18 wameumia kwenye tukio hilo.
Social Plugin